Lissu kusalia korokoroni hadi Juni 16, baada ya kesi kuahirishwa

Mwanasiasa huyo alifikishwa Mahakamani mapema Jumatatu akiwa chini ya ulinzi mkali.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kesi inayomkabili Mwenyekiti wa chama cha upinzani nchini Tanzania,Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Tundu Lissu, imeahirishwa hadi tarehe 16 mwezi huu .

Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama ya Kisutu Franco Kiswaga,ametoa uamuzi huo leo Jumatatu wakati wa kutajwa kwa kesi ambayo Lissu anashtakiwa kwa kosa la uhaini.

Aidha Lissu ameonywa dhidi ya kutamka maneno ovyo akiwa kizimbani baada ya kupayuka “No reform, no election” akiwa mahakamani.

Mwanasiasa huyo alifikishwa Mahakamani mapema Jumatatu akiwa chini ya ulinzi mkali.

Baadhi ya Wanachama wa CHADEMA, walizuiliwa kuingia ndani ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia kesi ya Lissu.

Lissu anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 3, mwaka huu, jijini Dar es Salaam, ambapo anadaiwa kutoa maneno ya uchochezi kwa lengo la kushawishi umma kuzuia kufanyika kwa Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.

Share This Article