Leonard Wamuthende ashinda kiti cha eneo bunge la Mbeere Kaskazini

Tom Mathinji
1 Min Read

‎Mwaniaji wa kiti cha ubunge cha Mbeere Kaskazini wa chama cha UDA Leonard Wamuthende, ametanganzwa mshindi baada ya kupata kura 15,802 na kumshinda mpinzani wake wa karibu Newton Karish wa chama cha DP.

‎‎Akitangaza matokeo hayo afisa msimamizi wa uchaguzi wa Mbeere Kaskazini John Kinyua, alisema wapiga kura 34,134 wakijitokeza dhidi ya wapiga kura 55,124 waliosajiliwa katika eneo bunge  hilo, ikiwa ni asilimia 61.92.

‎‎Mbunge huyo mteule baadaye alikabidhiwa cheti na tume ya IEBC.

‎Walioandamana na Wamuthende kupokea cheti chake ni pamoja na Naibu Rais Kithure Kindik, Waziri wa Utumishi wa Umma Geoffrey Ruku na Gavana wa Embu Cecily Mbarire.

‎Kiti hicho kilisalia wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa eneo hilo Geoffrey Ruku kuchaguliwa kwenye Baraza la Mawaziri.

‎Ushindi huo unahitimisha joto la kisiasa  ambalo limeshuhudiwa katika eneo bunge la Mbeere Kaskazini  katika siku za hivi majuzi.

Share This Article