Lamine Yamal aongeza mkataba na Barca hadi mwaka 2031

Akiwa na Barca,Yamal alitwaa mataji ya La Liga, Copa del Rey, na kombe la Super .

Dismas Otuke
1 Min Read

Wing’a matata wa Uhispania Lamine Yamal,amesaini mkataba mpya wa miaka siata na klabu ya  Barcelona, baada ya kuwasaidia kutwaa mataji matatu msimu huu.

Yamal aliye na umri wa miaka 17, alipachika mabao 18 na kuchangia kufungwa kwa mengine 25, katika mechi 55, alizowachezea Katalunya msimu uliomalizika wiki jana.

Akiwa na Barca,Yamal alitwaa mataji ya La Liga, Copa del Rey, na kombe la Super .

Aliichezea Barca kwa mara ya kwanza akiwa na umri wa miaka 15, akitokea akademia ya La Masia, alikojiunga akiwa na umri wa miaka saba .

 

Share This Article