Lagat hayuko huru katika mauaji ya Ojwang, yasema IPOA

Marehemu Ojwang’ aliaga dunia katika hali tatanishi Juni 8 mwaka huu akiwa mikononi mwa polisi wa kituo cha Central.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mamlaka Huru ya Kuchunguza Mienendo ya Polisi (IPOA), imekanusha madai yaliyozagaa katika baadhi ya vyombo vya habari kuwa imemwondolea lawama Naibu Inspekta Mkuu wa Polisi aliyejiondoa ofisini Eliud Lagat.

IPOA katika taarifa kwa vyombo vya habari na umma iliyochapishwa na mwenyekiti wake Ahmed Issack Hassan, imesema uchunguzi kuhusu mauaji ya mwanablogu Albert Ojwang bado unaendelea.

Marehemu Ojwang’aliaga dunia katika hali tatanishi Juni 8 mwaka huu akiwa mikononi mwa polisi wa kituo cha Nairobi Central.

IPOA imetaka umma kupuuzilia mbali madai hayo kuwa Lagat hana hatia na kuahidi kuwa inaendelea na uchunguzi, na iwapo atapatikana kuhusika katika mauaji hayo itatoa mapendekezo mwafaka ya kuadhibiwa kwake.

Share This Article