KUPPET yataka shule za msingi za JS kujisimamia

Martin Mwanje
1 Min Read
Akello Misori - Katibu Mkuu wa KUPPET

Chama cha Walimu wa Shule za Sekondari na Vyuo, KUPPET kaunti ya Laikipia kimesisitiza umuhimu wa shule za msingi za JS kujisimamia wakisema tofauti za viwango vya elimu kati ya wasimamizi wa shule za msingi na walimu wa JS zinaleta mvutano mkubwa baina yao.

Wakiongozwa na Katibu wa chama hicho katika kaunti ya Laikipia Robert Miano, walimu hao wanasema mgao wa fedha kwa shule umekuwa ukielekezwa sana kwa shule za msingi na kukosa kukidhi mahitaji muhimu ya JS.

Walimu hao wanasema sio haki kuona kwamba walisomea kufundisha kama wale wa sekondari na kwamba wanafanya kazi sawa, ilhali ifikapo kwa usimamizi, wanasimamiwa na wale wa shule za msingi.

Wanapendekeza kuwa wanafaa kupewa uhuru wa kujisimamia ili kuangazia na kusuluhisha changamoto zinazokumba elimu na walimu wa JS nchini.

TAGGED:
Share This Article