KUPPET yapinga kuondolewa kwa marupurupu ya Walimu 

Misori alisema hakuna utafiti wowote ambao umefanywa na serikali kudhihirisha kuwa maeneo hayo 44 yameimarika na itakuwa makossa kuondolea kwa marupurupu.

Dismas Otuke
2 Min Read
Mgomo wa walimu wa KUPPET wasimamiswa na mahakama.

Chama cha Walimu wa shule za sekondari na vyuo nchini (KUPPET), kimepinga vikali mapendekezo ya serikali ya kupunguza marupurupu ya maeneo yaliyo na mazingira magumu ya kufanya kazi kwa wanachama wake.

Akiwahutubia Wanahabari jana, Katibu Mkuu wa KUPPET, Akelo Misori, alisema wataenda mahakamani kupinga mpango huo wa serikali uliotangaza na Waziri mwenye mamlaka Musalia Mudavadi, alipofika bungeni wiki jana.

Mudavadi alisema kuwa serikali imepanga kuondoa maeneo 44 nchini yaliyoorodheshwa na tume ya kuwaajiri walimu -TSC ,katika orodha ya sehemu zenye mazingira magumu ya kufanya kazi, hivyo basi kufutilia mbali marupurupu wanayopokea walimu katika maeneo hayo kwa sasa.

Akiwa bungeni wiki jana, Mudavadi, alisema hatua hiyo itaokoa shilingi bilioni 6 kati ya bilioni 25, inazolipa kila mwaka kwa marupurupu hayo ya utendakazi katika mazingira magumu.

Misori alisema hakuna utafiti wowote ambao umefanywa na serikali kudhihirisha kuwa maeneo hayo 44 yameimarika na itakuwa makossa kuondolea kwa marupurupu.

Aidha, wameikosoa serikali wakitaja uamuzi huo kuwa wa haraka na usiostahili .

Baadhi ya maeneo yanayopendekezwa kuondolewa na serikali kama yenye mazingira magumu kwa walimu ni Chepalungu, Chonyi, Nyatike West, Nyatike North, Nyatike South, Rachuonyo North , Bomet, Kilifi na Migori .

KUPPET wameshikilia msimamo kuwa badala yake serikali inapaswa kuongeza maeneo yenye mazingira magumu ya kufanya kazi nchini .

Share This Article