KTDA yazindua mpango wa kuinua wakulima wadogo

Dismas Otuke
1 Min Read

Halmashauri ya ustawi wa majani chai nchini (KTDA), imezindua mkakati wa kuboresha kilimo na maisha ya wakulima wadogo wadogo.

Shughuli hiyo ambayo ilifanyika alhamisi katika hoteli ya Safari Park jijini Nairobi, ilihudhuriwa na wageni waalikwa 800, wakiwemo wakurugenzi wa matawi mbalimbali ya KTDA, maafisa wa serikali , benki kadhaa, kampuni za bima na wengine.

Mpango huu ni hatua ya kwanza kuhakikisha maslahi ya wakulima wadogo yanashughulikiwa ipasavyo.

Miongoni mwa yale yaliyopewa kipaumbele ni faida ya mazao ya, bima ya wakulima, mbinu na mikakati ya ukulima, uboreshaji wa bidhaa za chai na soko zaka, ushirikiano katika utendakazi baina ya wakulima, KTDA na washirika wengine.

Akihutubia hafla hiyo, mwenyekiti wa shirika hilo Chege Kirundi, alisema kuwa analenga kuleta mabadiliko muhimu katika shirika hilo.

“Lengo langu ni kuongoza mabadiliko ya uvumbuzi, usimamizi dhabiti na mazingira mazuri ya utendakazi kwa vizazi vijavyo. KTDA lazima iwe nguzo kuu ya wakulima’’ alisema Chege.

Zaidi ya hayo, KTDA ilizindua jarida la kila mwaka litakalotoa taarifa kwa wakulima kuhusu mipango na maendeleo ya KTDA, kama njia mojawapo ya kufanikisha malengo husika.

TAGGED:
Share This Article