KRA yawafurusha wafanyakazi 19 kwa kushiriki ufisadi

Tom Mathinji
2 Min Read
Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) Abdi Mohamud (Kushoto) na Kamishna MKuu wa KRA  Humphrey Wattanga (kulia)

Halmashauri ya ukusanyaji ushuru hapa nchini (KRA), imesema iliwatimua wafanyakazi 19 zaidi waliojihusisha na ufisadi katika kipindi cha nusu ya pili ya mwaka, kilichokamilika mwezi Disemba mwaka 2024.

Idadi hii ni maradufu ya wafanyakazi waliosimamishwa kazi na halmashauri hiyo mwaka uliotangulia, ambapo wafanyakazi 9 walifutwa kazi.

Akizungumza wakati wa mkutano na Afisa Mkuu Mtendaji wa Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) Abdi Mohamud, Kamishna MKuu wa KRA  Humphrey Wattanga, alisema taasisi hizo mbili zimeshirikiana katika usambazaji habari za kijasusi, uchunguzi wa pamoja na kubuni mikakati ya pamoja kukabiliana na changamoto zinazosababishwa na ufisadi na ukwepaji kulipa ushuru.

“Hatuwezi wapuuza wale ambao wanahujumu mifumo yetu. Ushirikiano wetu na EACC ni muhimu zaidi. Tutabuni mikakati thabiti ya kutambua ukwepaji kulipa ushuru na kuweka adhabu kali kwa wale wanaofanikisha ukwepaji huo,” alisema Wattanga.

Wakati wa kipindi hicho cha nusu ya pili ya mwaka, onyo kwa wafanyakazi zilipungua hadi mbili kutoka 15, kuashiria hatua ya KRA ya kukabilioana na ufisadi vilivyo.

Kwa upande wake Mohamud alisema ushirikiano huo ni muhimu katika juhudi za kutokomeza zimwi la ufisadi na kukumbatia uzingatiaji wa sheria.

“Pamoja tunaweza buni mazingira yasiyovumilia ufisadi, ukwepaji kulipa ushuru, lakini tuwe na mazingira yanayopigia debe maadili bora ya kufanya biashara,” alisema Mohamud.

TAGGED:
Share This Article