Korongo wa Uganda wakataa abadan kufurushwa CHAN mapema

Uganda walimaliza wa kwanza kwa pointi 7 ,moja zaidi ya Algeria na Afrika Kusini.

Dismas Otuke
1 Min Read

Wenyeji wenza wa fainali za kombe la CHAN Uganda Cranes, walikataa kata kata kutimuliwa mashindanoni mapema, baada ya kulazimisha sare ya 3-3, dhidi ya Bafana Bafana kutoka Afrika Kusini.

Mechi hiyo  ya mwisho ya kundi C ilisakatwa  Jumatatu usiku uwanjani Nelson Mandela  huku Crannes wakifuzu kwa kwota fainali kwa mara ya kwanza na kujiunga na majirani na waandalizi wenza Kenya na Tanzania.

Jude Ssemugabi alifungua ukurasa wa magoli kwa wenyeji dakika ya 31, kabla ya Ramahlwe Mphahlele, kusawazishia Afrika kusini dakika ya 53, na kisha baadaye Thabiso Kutumela, akawaweka uongozini  dakika 5 baadaye.

Afrika Kusini waliongeza goli la tatu  lake Ndabayithethwa Ndlondlo dakika 12 kabla ya kipenga cha mwisho.

Allan Okello alikomboa goli moja kwa akina Ssebo dakika ya 87, kupitia penati naye Rogers Torach. akapiga la tatu kunako  dakika ya 9,6 na kuwapa Cranes sare waliyohitaji kuongoza kundi hilo.

Uganda walimaliza wa kwanza kwa pointi 7 ,moja zaidi ya Algeria na Afrika Kusini.

Share This Article