Korea Kaskazini yahifadhi Kombe la Dunia wanawake chini ya miaka 17

Dismas Otuke
1 Min Read

Korea Kaskazini ilikuwa na wakati rahisi kabla ya kuhifadhi kombe la Dunia kwa wanawake wasiozidi umri wa miaka 17 baada ya kuichabanga Uholanzi mabao 3-0 kwenye fainali iliyosakatwa jijini Rabat,Morocco.

Kim Won im,PAK Rye Yong na RI Ui Gyong walipachika magoli ya Korea kunako dakika za 14,18 na 42 huku wakitwaa taji hiyo kwa mara ya nne.

Mexico waliishinda Brazil kupitia penati na kumaliza katika nafasi ya tatu kufuatia sare ya bao 1-1.

Share This Article