Kombe la kifahari la Ligi ya bingwa barani Ulaya (UEFA Champions League) limewasilishwa Kenya katika ziara amabyo pia litazungushwa katika mataifa tano ya Vietnam, Indonesia, Afrika Kusini, Zambia na Kenya.
Ziara hiyo inayofadhiliwa na kampuni ya Heinken inaongozwa na aliyekuwa kiungo mkabaji wa klabu za Manchester United na Bayern Munich -Bastian Schweinsteiger,na inalenga kuwapa wapenzi wa soka nchini fursa ya kutazama kombe hilo .
Mapema Ijumaa Schweinsteiger, aliyeshinda taji hiyo mwaka 2013 na Bayern Munich, aliwasilisha kombe kwa wanahabari katika hoteli ya Serena jijini Nairobi..
Baadaye Leo, kombe hilo liliwasilishwa kwa Rais William Ruto katika ikulu ya Nairobi kwenye hafla iliyohudhuriwa na maafisa wa wizara ya michezo, shirikisho la kandanda nchini ( FKF), Kenya wines Agency limited ( KWAL), Kampuni ya Heineken na UEFA.
Kesho jumamosi, Heineken na FKF wataandaa kikao na vigogo wa kabumbu humu nchini watakaotangamana na Schweinsteiger.
Aidha Mashabiki 700 wa kwanza watapata fursa ya kutazama na kupiga picha na kombe hilo.
Ziara hii amabayo ilianza tarehe saba Aprili nchini Vietnam, na inakamilikia hapa nchini,na inalenga kuwapa mashabiki na wadau wa soka fursa ya kutangamana, kabla ya fainali ya Makala ya mwaka huu itakayogaragazwa ugani Alianz Arena, nchini Ujerumani tarehe 31 mwezi huu.