Kombe la kifahari la CHAN liko jijini Nairobi tayari kukabidhiwa mshindi Jumamosi hii katika uwanja wa Kasarani wakati wa fainali.
Kiungo na nahodha wa zamani wa Harambee Stars Victor, ambaye ni balozi wa CHAN, aliongoza msafara wa maafisa wa shirikisho la soka, CAF uliozuru KBC mapema leo Jumatatu na kuandamana na kombe hilo.
Wanyama alisifia fainali hizo kutokana na mchango mkubwa wa kukuza vipaji kwa wachezaji.
Msafara wa kombe hilo uliongozwa na Wanyama na ulipokelewa na Mkurugenzi Mkuu wa KBC, Agnes Kalekye.
Aidha, Wanyama alipongeza mchango wa mashabiki kupamba mashindano hayo.
Kipute cha CHAN kitaingia nusu fainali Jumanne wiki hii kwa mechi kati ya Madagascar dhidi ya Sudan kuanzia saa kumi na moja unusu jioni, kabla ya Morocco kumaliza udhia na ya Senegal saa mbili unusu usiku.