Kiunjuri azitaka jamii za Trans Nzoia kuishi kwa amani

Martin Mwanje
1 Min Read
Mwangi Kiunjuri - Mbunge wa Laikipia Mashariki

Mbunge wa Laikipia Mashariki Mwangi Kiunjuri amehimiza jamii ya Agikuyu wanaoishi kaunti ya Transnzoia kuishi kwa amani pasi ya kugawanywa kwa misingi ya kikabila

Akizungumza katika kaunti ya Transnzoia alipokutana na jamii hiyo, mbunge huyo ametaka wakazi wa kaunti hiyo kuishi kwa amani na kujiepusha na siasa kwani kile wanachopaswa kuitisha ni maendeleo.

Hata Hivyo, viongozi wa eneo hilo wakiongozwq na Paul Kanya wameitaka serikali kuwapatia maendeleo na kuahidi kujiepusha na siasa chafu zinazoweza kutishia ustawi wa kaunti hiyo.

Share This Article