Huku ugonjwa wa Saratani ukisalia kuwa changamoto kuu hapa nchini, wizara ya Afya inajizatiti kuhakikisha inakabiliana na ugonjwa huo kwa kubuni vituo vya uchunguzi na matibabu kote nchini.
Wakazi wa Samburu ndio wa hivi punde kunufaika na kituo cha matibabu ya Saratani, kilichofunguliwa rasmi na waziri wa Afya Dkt. Deborah Barasa katika hospitali ya rufaa ya kaunti ya Samburu.
“Kituo hiki kitatoa matibabu ya Saratani kwa wakazi wa Samburu na kuwapunguzi mzigo wa kusafiri mwendo mrefu kutafuta matibabu hayo,” alisema Dkt. Barasa kupitia ukurasa wa wizara hiyo wa X.
Kulingana na waziri huyo, kliniki hiyo itahakikisha wagonjwa wa Saratani wanahudumiwa chini ya mpango wa afya wa Taifa Care, na hivyo kuleta matibabu maalum karibu na wananchi.
Waziri huyo aliwatembelea kina mama wajawazito na kituo cha watoto waliozaliwa, kuhakikisha wamesajiliwa katika mpango wa SHA.