Mwanamume mmoja wa umri wa miaka 20 kutoka eneo la Amagoro, eneo bunge la Kiminini katika kaunti ya Trans Nzoia anaendelea kupokea matibabu baada ya kupatikana na ugonjwa wa Mpox huku kijiji kimoja kikishukiwa kuathiriwa mno na ugonjwa huo.
Kulingana na Waziri wa Afya wa kaunti ya Transnzoia Sam Ojwang, kisa hicho cha maambukizi kilithibutisha kuwa ugonjwa wa Mpox baada ya kuchukua sampuli za mgonjwa huyo na kupelekwa kupima katika maabara kuu jijini Nairobi.
Ojwang ameomba umma kuepuka kuwatia hofu wakazi kwani ugonjwa huo unaweza kudhibitiwa na kuwaonya wakazi kuchukua hatua za kuepukana na maambukizi.
Mgonjwa huyo tayari anaendelea kupokea matibabu huku juhudi za kufuatilia yeyote aliyetangamana naye zikiendelea.