Kipyegon na Chebet watuzwa shilingi milioni 5 na Serikali

Waziri wa Michezo Salim Mvurya, aliwatuza wanariadha hao baada ya kukutana nao katika afisi za Talanta Plaza mepema leo.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Olimpiki Faith Kipyegon na Beatrice Chebet wametuzwa shilingi milioni 5 kila mmoja na wizara ya Michezo, baada ya kuvunja rekodi za dunia Jumamosi iliyopita .

Waziri wa Michezo Salim Mvurya, aliwatuza wanariadha hao baada ya kukutana nao katika afisi za Talanta Plaza mepema leo.

Kipyegon pia  alivunja rekodi ya dunia ya mita 5000 akisajili dakika 13 sekunde 58.68 ,akivunja rekodi ya awali ya Gudat Tsegay ya dakika 14.21, iliyowekwa mwaka 2023.

Kipyegon na Chebet walirejea nchini jana usiku kutoka Eugene Marekani , waliposhiriki mashindano ya Prefontaine Classic Diamond League.

Share This Article