Kipyegon na Chebet kurejea nyumbani leo usiku kutoka Marekani

Kipyegon alivunja rekodi yake ya mita 1500 ya mwaka uliopita akiweka rekodi mpya ya dakika 3 sekunde 48.68.

Dismas Otuke
1 Min Read

Mabingwa wa Olimpiki Faith Kipyegon na Beatrice Chebet, wanatarajiwa kurejea nyumbani leo usiku kutoka Eugene,Marekani walikovunja rekodi za dunia Jumamosi iliyopita.

Kipyegon alivunja rekodi yake ya mita 1500 ya mwaka uliopita akiweka rekodi mpya ya dakika 3 sekunde 48.68.

Chebet ambaye ni mshindi wa dhahabu mbili za Olimpiki aliweka rekodi mpya ya mita 5000 ya dakika 13 sekunde 58.06 ,akivunja rekodi ya mwaka 2023 ya Gudaf Tsegay ya dakika 14 nukta 2.

Kipyegon atakuwa katika kundi la kwanza la wanariadha watakaowasili kwa ndege ya shirika la KLM saa nne kamili usiku,wakati Chebet akitarajiwa kutua saa sita kasoro dakika 10 usiku kwa ndege ya Qatar Airways.

Share This Article