Kipyegon alenga kuvunja rekodi ya Dunia ya Maili moja leo usiku

Kipyegon, ambaye pia ni bingwa mara tatu wa Dunia, atalenga kukimbia maili moja chini ya dakika 4.

Dismas Otuke
1 Min Read

Bingwa mara tatu wa Olimpiki Faith Kipyegon, atalenga kuvunja rekodi ya Dunia ya maili moja katika shindano la kampuni ya Nike la Breaking4, leo usiku nchini Ufaransa.

Kipyegon, ambaye pia ni bingwa mara tatu wa Dunia, atalenga kukimbia maili moja chini ya dakika 4.

Mwanariadha huyo mwenye umri wa miaka 31 anashikilia rekodi ya maili moja ya dakika 4 sekunde 7.64, aliosajili mwaka 2023 mjini Monaco, Ufaransa.

Kipyegon atasaidiwa na wapiga kasi pamoja na mitambo ya kielektroniki kwenye jaribio lake la kuwa mwanamke wa kwanza kukumbia maili moja chini ya dakika 4.

Share This Article