Kipute cha Kombe la Dunia kwa Vilabu kurejea kwa robo fainali

Fluminense ya Brazil, watakumbana na miamba wa Saudi Arabia Al Hilal, kuanzia saa nne usiku

Dismas Otuke
1 Min Read

Kindumbwendumbwe cha Kombe la Dunia baina ya vilabu kitatarejea leo kwa mechi za robo fainali baada ya mapumziko ya siku moja.

Fluminense ya Brazil, watakumbana na miamba wa Saudi Arabia Al Hilal, kuanzia saa nne usiku katika uwnaja wa Camping World mjini Orlando.

Mapema kesho waakilishi wengine wa Brazil, Palmeiras watapimana ubabe na Chelsea ya Uingereza saa kumi alfajiri Lincoln Financial mjini Philadelphia.

Baadaye saa moja usiku mabinwga wa Ulaya PSG, watakuwa na mtihani mgumu  dhidi ya Bayern Munich ya Ujerumani katika uchanjaa wa Mercedez Benz mjini Georgia .

Real Madrid kutoka Uhispania watashuka uwanjani Metlife mjini East Rutherford, kuanzia saa tano katika kwota fainali ya ya mwisho  dhidi ya Borusia Dortmund.

Mabingwa wa kombe hilo watatuzwa donge nino la shilingi bilioni 16.256.

Share This Article