Kiplimo avunja rekodi ya dunia ya nusu marathon mjini Barcelona

Dismas Otuke
1 Min Read

Mganda Jacob Kiplimo ameweka rekodi mpya ya dunia katika mbio za nusu marathon ya dakika 56 na sekunde 42 ,kwenye makala ya mwaka huu ya mbio za eDreams Mitja Marató Barcelona by Brooks, zilizoandaliwa Jumapili asubuhi.

Bingwa huyo mara mbili wa dunia katika mbio za nyika amefutilia mbali rekodi ya awali ya dunia iliyokuwa ikishikiliwa na Mwethiopia Yomif Kejelcha ya dakika 57 na sekunde 30, akiiboresha kwa sekunde 48.

Kiplimo aliye na umri wa miaka 24 aliongoza mbio hizo akifuatwa na Wakenya Geofrey Kamworor na Samuel Mailu waliomaliza katika nafasi za pili na tatu kwa dakika 58 na sekunde 44 na dakika 59 na sekunde 40 mtawalia.

TAGGED:
Share This Article