Kipa mstaafu na aliyekuwa nahodha wa timu ya taifa ya Nigeria maarufu kama Super Eagles, Peter Rufai alifariki mapema jana Julai 3, akiwa na umri wa miaka 61.
Rufai alifariki akipokea matibabu katika hospitali moja mjini Lagos, baada ya kulazwa kwa muda mrefu.
Rufai aliichezea Super Eagles kwa kipindi cha miaka 17, kuanzia mwaka 1981 akipiga jumla ya mechi 65 .
Marehemu alishiriki fainali za Kombe la Dunia za mwaka 1994 na 1998 na fainali tatu za AFCON na kunyakua kombe la Afrika na Super Eagles mwaka 1994.