Kiongozi wa chama cha upinzani nchini Congo cha The Socialistes Congolais-Lassy Mbouity, na mwaniaji wa uchaguzi wa Urais wa mwezi Machi mwaka ujao wametekwa nyara na kundi la watu wasiojulikana.
Yamkini wawili hao waliripotiwa kutekwa nyara na kundi la watu waliojihami na kufunika nyuso zao Jumapili iliyopita mjini Brazzaville, siku chache baada ya Mbouity kuepuka jaribio la kuawa.
Wanasiasa wa upinzani nchini Congo na mashirika ya haki za kibinadamu yalijitokeza kukashifu utekaji nyara huo, yakitaka serikali kukomesha uovu.