Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki ametetea mpango unaoendelea wa kuwawezesha Wakenya hasa vijana na wanawake katika maeneo mbalimbali ya nchi.
Prof. Kindiki amekuwa akiongoza viongozi kadhaa wa utawala wa Kenya Kwanza kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi na kuzindua mpango unaokusudia kuwawezesha Wakenya kujikimu kimaisha kupitia vikundi vyao.
“Kama kuna watu hawataki program ya empowernment, wakuje hapa waseme mchana, wasiseme kwa mtandao. Wakuje hapa Maragua, waseme empowerment ni mbaya,” alisema Naibu Rais wakati akiwahutubia wakazi akiwa ameandamana na viongozi mbalimbali.
“Wakuje waseme mbele yenu, waseme hii empowerment haina maana. Kwa hivyo sisi, for the time being, kwa sababu mmetuambia hii empowerment ni muhimu, kwa sasa tutaendelea na hii empowerment.”

Matamshi yake yanakuja wakati viongozi wa upinzani wamekosoa vikali mpango huo wakidai ni njama ya kushawishi raia kwa kutumia fedha za umma kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2027.