Ronald Kimeli Kurgat na Gladys Chemutai washindi wakilomita 42 katika makala ya 21 ya mbio za Standard Chartered Nairobi Marathon zilizoandaliwa mapema Jumapili.
Kurgat aliziparakasa mbio hizo kwa muda wa saa 2 dakika 13 na sekunde 5,akifuatwa na Dominic Kipkurui kwa saa 2 dakika 13 na sekunde 13, huku Peter Kwemoi Ndorobo akiridhia nafasi ya tatau kwa saa 2 dakika 14 na sekunde 14.
Glady Chemutai Chemutai alitwaa ubingwa katika marathon ya wanawake akitumia saa 2 dakika 31 na sekunde 52 ,akiafuatwa na Caroline Koech kwa muda wa saa 2 dakika 35 huku Joy Kemuma akiridhia nafasi ya tatu kwa saa 2 dakika 36 na sekunde 6.

Kurgat na Chemutai watapokea tuzo ya shilingi milioni 2 kila mmoja kwa ushindi huo.
Matokeo ya Kilomita 42 wanaume
1 Ronald Kimeli Kurgat KEN 2:13:05
2 Dominick Kipkirui KEN 2:13:13
3 Peter Kwemoi Ndorobo KEN 2:13:14
4 Richard Rop KEN 2:13:21
5 John Mburu Muiruri KEN 2:13:46
Matokeo ya Kilomita 42 wanawake
1 Gladys Chemutai KEN 2:31:52
2 Caroline Koech KEN 2:35:00
3 Joy Kemuma KEN 2:36:06
4 Ruth Wakabu KEN 2:37:49
5 Sheila Chepkech KEN 2:41:57
Vincent Mutai na Gladys Koech wameshinda kilomita 21 kwa wanaume na wanawake mtawalia.
Mutai ameibuka mshindi baada ya kuzitimka kwa saa 1 dakika 3 sekunde 27,akifuatwa na Keyborn Obato kwa saa 1 dakika 3 na sekunde 34, huku Silas Kiplimo, akiambulia nafasi ya tatu kwa saa 1 dakika 3 na sekunde 51.
Koech ameibuka mshindi katika nusu marathon ya wanawake akitumia saa 1 dakika 12 na sekunde 10,akifuatwa na Esther Chemutai kwa saa 1 dakika 12 na sekunde 12, huku Mercy Jerotich akimaliza wa tatu kwa saa 1 dakika 13 na sekunde 59.