Kikosi cha pili cha Kenya chaelekea Tokyo kwa mashindano ya Riadha Duniani

Makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani yataandaliwa kati ya Jumamosi hii Septemba 13 na 21 huku Kenya ikiwakilishwa na wanariadha 58.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kikosi cha pili cha timu ya Kenya kimeondoka nchini Jumatano jioni kuelekea Tokyo, Japan, kushiriki mashindano ya Riadha Duniani kuanzia Jumamosi hii.

Wanariadha waliosafiri kwa kutumia ndege ya Qatar Airways ni pamoja na bingwa wa Olimpiki katika mita 800 Emmanuel Wanyonyi, bingwa wa dunia wa mita 800 kwa chipukizi Sarah Moraa, Nicholas Kebenei, Kelvin Kimtai, Alex Ngéno, Lillian Odira na Vivian Kiprotich, wote wa mita 800.

Wengine ni washiriki wa mbio za mita 5,000, mshindi wa nishani ya shaba mwaka 2023 Jacob Krop, Cornelius Kemboi na Mathew Kipsang.

Makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani yataandaliwa kati ya Jumamosi hii Septemba 13 na 21 huku Kenya ikiwakilishwa na wanariadha 58.

Share This Article