Kocha mkuu wa timu ya taifa Harambee Stars, Benni McCarthy, ametaja kikosi cha mwisho cha wanandinga 25 watakaoshiriki fainali za kombe la CHAN mwezi ujao.
McCarthy ameajumuisha wachezaji wenye tajiriba na chipukizi huku Kenya ikishiriki fainali za CHAN kwa mara ya kwanza.
Fainali za CHAN zitaandaliwa kwa pamoja na Kenya, Uganda na Tanzania pamoja na Zanzibar kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu.
Makipa
Faruk Shikhalo, Byrne Omondi, Sebastian Wekesa
Mabeki
Siraj Mohammed, Manzur Suleiman, Pamba Swaleh, Abud Omar, Alphonce Omija, Sylvester Owino, Mike Kibwage, Daniel Sakari, Lewis Bandi, Kevin Okumu
Viungo
Brian Musa, Alpha Onyango, Austin Odhiambo, Ben Stanley, Marvin Nabwire
Washambulizi
Mohammed Bajaber, Boniface Muchiri, David Sakwa, Ryan Ogam, Masoud Juma, Austin Odongo, Felix Oluoch
Kiranja wa kikosi atakuwa Aboud Omar akisaidiwa na Daniel Sakari na Alphone Omija.
Kenya imejumuishwa kundi A pamoja na miamba Morocco, DR Congo, Zambia na Angola, huku wakifungua dimba dhidi ya DRC tarehe 3 mwezi ujao ugani Kasarani.