Kenya yatafuta usaidizi wa Luxembourg kuimarisha Jiji la Nairobi

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Mudavadi, ashiriki mazungumzo na Naibu Waziri Mkuu wa Luxembourg Xaver Bettel.

Waziri mwenye Mamlaka Makuu aliye pia Waziri wa Mambo ya Nje Musalia Muadavadi, ametafuta  usaidizi wa Luxembourg ili kuimarisha nafasi ya Jiji la Nairobi kama Makao ya shirilka la Umoja wa Mataifa kuhusu Mazingira (UNEP).

Katika mkutano na Naibu Waziri Mkuu wa Luxembourg Xaver Bettel, Minister of Foreign Affairs and Foreign Trade of Luxembourg, Muadavadi alielezea hatua za kijasiri zilizochukuliwa za kupiga marufuku matumizi ya plastiki nchini, huku akielezea kujitolea kwa Kenya kutekeleza hatua za kuhifadhi mazingira.

Mudavadi alizungumzia jinsi hadhi inayoimarika ya Jiji la Nairobi katika ngazi za kimataifa itadhihirika zaidi, litakapoandaa kwa pamoja kongamano la Bara Afrika na Ufaransa mwezi Mei mwaka 2026, ambapo itakuwa mara ya kwanza kwa kongamano hilo kuandaliwa nje ya ufaransa au taifa la kiafrika linalozungumza kifaransa.

Walikubaliana kuimarisha uhusiano na kuihimiza Luxembourg kuanzisha ujumbe wa kidiplomasia jijini Nairobi ili kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizi mbili.

Musalia pia aliihimiza Luxembourg kuunga mkono juhudi za Kenya za kuondolewa kwenye orodha ya jopo la kukabiliana na ulanguzi wa fedha akibainisha marekebisho ya kisheria na kitaasisi ambayo tayari yametekelezwa na kuzungumzia kuhusu ripoti ya shirika la fedha duniani kuhusu tathmini ya uongozi baadaye mwaka huu.

Share This Article