Kenya imeshuka kutoka nafasi 126 hadi nafasi ya 127, katika orodha ya viwango vya ubora wa usalama duniani vya mwaka 2025.
Kwa mujibu wa takwimu za Global Peace Index ,viwango vya usalama vya Kenya vimedorora kutoka nambari 126 iliyokuwa ikishikilia mwaka 2024, kati ya mataifa yote 163 yaliyoorodheshwa.
Viwango vya usalama hushuka au kuwa bora kwa kuzingatia shinikizo za ndani na kutoka nje ya nchi.
Tanzania imeorodheshwa bora Afrika Mashariki katika nafasi ya 73,ikifuatwa na Rwanda iliyo ya 91 wakati Uganda ikiwa ya 113 kisha Burundi inakalia nafasi ya 133.