Kenya yarushwa kundi moja na Senegal AFCON U20

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya kwa chipukizi walio chini ya umri wa miaka 20, imejumuishwa kundi C katika fainali za kuwania kombe la AFCON mwaka huu nchini Côte d’Ivoire.

Kenya imejumuishwa pamoja na mabingwa watetezi Senegal,Zambia na Sierra Leone.

Kundi A lina wenyeji Côte d’Ivoire, Ghana, Tanzania, na timu moja itakayofuzu kutoka Afrika Kaskazini.

Morocco, Afrika Kusini, Misri,na Nigeria zimejumuishwa kundi C.

Kipute hicho kitaandaliwa kati ya Aprili 26 na Mei 18 mwaka huu.

Share This Article