Kenya imejipatia soko jipya la kuuza chai na kahawa nchini Morocco, kufuatia ziara ya hivvi maajuzi ya serikali ya Kenya ilipofungua ubalozi mjini Rabat.
Akizungumza wakati wa kufungua rasmi ubalozi wa Kenya mjini Rabat,Waziri aliye na mamlaka Musalia Mudavadi, alisema anaamini kuwa mkakati uliowekwa na Morocco, ni dhabiti kwa kusuluhisha utata wa Sahara Magharibi.
Kufuatia msimamo huo Kenya sasa iko huru kuuza kahawa na chai kwa taifa hilo la kaskazini mwa Afrika.
Kenya imekuwa ikiuza bidhaa za dhamani ya shilingi nusu bilioni kila mwaka nchini Morocco, huku ikiagiza bidhaa za shilingi bilioni 12 kwa mwaka kutoka Morocco.