Serikali ya Kenya imekariri kujitolea kuhakikisha usalama wa wagonjwa kama nguzo muhimu ya afya kwa wote kuwalinda watoto wachanga.
Akizungumza siku ya Jumanne alipoongoza maadhimisho ya siku ya kimataifa ya usalama wa wagonjwa katika hospitali ya chuo kikuu cha Aga Khan, Katibu wa Afya ya Umma Mary Muthoni, amesisitiza haja ya kutoa kipaumbele kwa usalama wa afya ya wagonjwa na hususan watoto wachanga.
Alitaja baadhi ya hatua zilizopigwa katika kupunguza magonjwa ya watoto wachanga na kupunguza idadi ya watoto wanaofariki wanaozaliwa na magonjwa ya kuambukiza.