Timu ya taifa Harambee Stars imeimarisha mazoezi yake kujiandaa kwa kipute cha kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN.
Harambee Stars wanashiriki kipute cha CHAN kwa mara ya kwanza huku wakipangiwa kufungua dimba dhidi ya DRC kundini A Jumamosi ijayo.
Mataifa mengine kundini hilo pamoja na Kenya ni Morocco, Zambia, na Angola.
DRC imekita kambi ya mazoezi nchini Tanzania ambapo pia inatarajiwa kucheza mchuano wa kujipima nguvu dhidi ya mabingwa watetezi wa CHAN Jumanne ijayo,kabla ya kusafiri kuja Nairobi.