Kenya na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) zimeahidi kuboresha ushirikiano katika sekta za kilimo na mifugo katika hatua inayolenga kuongeza faida kwa wakulima.
Hii ni kwa kuhakikisha wakulima wanapata masoko bora, rasilimali za kifedha, usafiri unaotosheleza na fursa za kibiashara za kikanda.
Ahadi hizo zimetolewa wakati wa mkutano kati ya Waziri wa Kilimo Mutahi Kagwe na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa WFP nchini Italia Valerie Guarnieri.
Wakati wa mkutano huo, Kagwe alisisitiza kujitolea kwa Kenya katika kuhakikisha usalama wa chakula na maendeleo endelevu.
Kagwe akitoa mfano wa hatua zinazochukuliwa na serikali ya Kenya kuunga mkono mipango muhimu ya WFP humu nchini ikiwa ni pamoja na misaada ya chakula na mipango ya lishe shuleni.
Kulingana na Waziri huyo, mipango hiyo hutekeleza wajibu muhimu katika kuboresha viwango vya elimu, afya na ustawi wa binadamu.