Timu ya taifa ya Kenya kwa wachezaji walio chini ya umri wa miaka 20-Rising Stars, ilibanduliwa kutoka fainali za Kombe la mataifa ya Afrika nchini Misri, roho juu baada ya kulazimisha sare ya 2-2 dhidi ya mabingwa mara saba, Nigeria, katika mechi ya kundi B jana usiku.
Sawia na mechi mbili za awali, Kenya walitangulia kufunga bao kunako dakika ya sita kupitia Kevin Wanganya, kabla Kparobo Arierhi, kusawazisha dakika ya 13.
William Gitamu aliwaweka Kenya ungozini tena dakika ya 68, lakini Nigeria wakasawazisha tena kupitia kwa penati iliyofungwa na Daniel Bameyi dakika ya 73.
Morocco walioizaba Tunisia mabaoa 3-1, waliongoza kundi hilo kwa alama, wakifuatwa na Nigeria kwa pointi 5 huku Tunisia, ikichukua nafasi ya tatu kwa alama 3 nayo Kenya ikashika mkia kwa pointi 1.