Kenya Pipeline wavuliwa ubingwa wa Zone V na APR

Dismas Otuke
0 Min Read

Kenya Pipeline walivuliwa ubingwa wa Zone 5 kwa wanawake baada ya kuambulia kichapo cha seti 3-1 kutoka kwa miamba wa Rwanda,Rwanda Patriotic Army (APR).

Vipusa wa KPC walinyakua seti ya kwanza alama 30-25,kabla ya kucharazwa seti tatu zilizofuatia 17-25,24-26 na 23-25.

Fainali hiyo iliandaliwa jana jioni katika ukumbi wa Lugogo jijini Kampala,Uganda.

TAGGED:
Share This Article