Kenya Pipeline waelekea Abuja kwa mashindano ya Afrika

Dismas Otuke
1 Min Read

Klabu ya Kenya Pipeline imondoka nchini  leo kuelekea Abuja,Nigeria kushiriki mashindano ya klabu bingwa Afrika kwa wananawake.

Pipeline wameratibiwa kushiriki mashindano ya Afrika kati ya April 1 na 14 .

Timu hiyo inayoongozwa na kocha Geofrey Omondi imekuwa mazoezini katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani kujiandaa kwa mashindano hayo.

Meneja Mkurugenzi wa kampuni ya KPC Joe Sang ameiaga rasmi timu hiyo leo akiipa changamoto ya kusajili matokeo mazuri na kuwa mabalozi wema.

Kocha Omondi pamoja na nahodha Gladys Ekaru,wamesema wamejiandaa vyema wakilenga matokeo bora.

Kikosi hicho kinawajumuisha maseta;Emmaculate Nekesa na Faith Imodia,washambulizi Noel Murambi na Loice Simiyu huku walinzi wa kati wakiwa Marian Sokoiyo, Trizah Atuka, Gladys Ekaru na Lydia Emokol nao Daisy Leting, Leonida Kasaya, Mariam Musa na Betty Sifuna huku Agrippina Kundu na Celestine Nafula wakiwa malibero.

Share This Article