Kenya na Japani zimeimarisha ushirikiano katika sekta ya afya kwenye kikao cha pamoja kati ya Waziri wa Afya Kenya Aden Duale, na mwenzake wa Japani Minoru Kiuchi.
Kikao hicho kilifanyika pembezoni mwa Kongamano la 9 la Tokyo kuhusu Maendeleo ya Afrika( TICAD 9) mapema leo Jumatano.
Kwenye mkutano huo, ilikubaliwa kuwa Kenya itaimarisha ushirikiano na Japani katika nyanja kama vile teknolojia ya afya, tabi anchi, mapambano dhidi ya magonjwa yasiyokuwa ya maambukizi, uzee na ufadhili wa afya.
Kikao hicho pia kilihudhuriwa na mshauri wa Rais kuhusu afya Dkt. Daniel Mwai, Mkurugenzi Mkuu wa Afya Dkt. Patrick Amoth na mwenyekiti wa Taasisi ya Utafiti wa Afya nchini KEMRI, Dkt. Abdullahi Ali.