Kenya na Italia zimedumisha uhusiano imara, asema Rais Ruto

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais William Ruto ashiriki mazungumzo na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni.

Kenya na Italia zimedumisha uhusiano imara kwa muda wa miaka 60 iliyopita, hayo ni kwa mujibu wa Rais William Ruto.

Akizungumza leo Jumatatu aliposhiriki meza ya mazungumzo na Waziri Mkuu wa Italia Giorgia Meloni pembezoni mwa  Mkutano wa Pili wa mifumo ya chakula ya Umoja wa Mataifa Jijini Addis Ababa, Ethiopia, kiongozi wa taifa alisema uhusiano huo umekuzwa kwa ushirikiano thabiti wa kidiplomasia, na hivyo kukuza msingi imara wa ushirikiano katika sekta mbalimbali.

“Uhusiano kati ya nchi hizi mbili umechochewa na ushirikiano mzuri wa raia, ukuaji wa biashara na uwekezaji na ushirikiano wa karibu katika masuala ya amani na usalama.

Rais Ruto alisema Italia imethibitisha kuwa mshirika thabiti wa Kenya, na imechangia pakubwa katika kuunga mkono ajenda ya kuleta mageuzi hapa nchini hasa kupitia upanuzi wa miundombinu ya Konza Technopolis na maendeleo katika mipango ya anga za juu ya Kenya.

Share This Article