Kenya na China zaimarisha ushirikiano kufanikisha maendeleo, asema Mudavadi

Tom Mathinji
1 Min Read
Waziri Mwenye Mamlaka Makuu Musalia Mudavadi.

Kenya na China zinaendelea kupanua ushirikiano baina yake kupitia kuimarisha uchumi na kukumbatia tamaduni ambazo zitainua maisha ya wananchi wa mataifa hayo mawili na kuboresha maendeleo ya bara la Afrika.

Mkuu wa Mawaziri Musalia Mudavadi alisema China imeonyesha mfano mwema hasaa kwa kuwaokoa mamilioni ya raia wake kutoka kwa lindi la ufukara hadi kuhakikisha ustawi wa kijamii na kuchukua usukani kufanikisha maendeleo, uongozi bora na  amani duniani.

Mudavadi alisema Kenya inazidi kujitolea kushirikiana kwa karibu na China kuimarisha ukuaji na ustawi wa pamoja kwa manufaa ya raia wa nchi hizo mbili.

Maadhimisho ya miaka 76 tangu kuanzishwa kwa taifa la China.

“Kenya inaheshimu uafiki uliopo kati yake na China pamoja na ushirikiano wenye manufaa chini ya jukwaa la ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC).

Waziri huyo wa Mambo ya Nje aliyasema hayo Jumatatu katika ubalozi wa China Jijini Nairobi, wakati wa maadhimisho  ya miaka 76 tangu kuanzishwa kwa Jamhuri ya Watu wa China.

Wakati wa maadhimisho hayo, Mudavadi alituma ujumbe wa heri njema kwa Rais Xi Jinping, serikali yake na watu wa China kutokana na juhudi zao za kutafuta ustawi na maelewano ulimwenguni.

Share This Article