Kenya na Chad zaumiza nyasi bila sababu

Kenya na Chad zitakuatana tena Jumanne ijayo kwa mchuano wa pili wa kirafiki.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars na Chad zimetoka sare tasa katika mechi ya kimataifa ya kirafiki iliyosakatwa Jumamosi jioni katika uwanja wa Marrakech nchini Morocco.

Kenya na Chad zitakuatana tena Jumanne ijayo kwa mchuano wa pili wa kirafiki.

Harambee Stars inatumia mechi hizo kujipiga msasa kwa fainali za Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za nyumbani maarufu kama CHAN, kati ya Agosti 2 na 30 mwaka huu nchini Tanzania,Uganda na Kenya.

Share This Article