Kenya kuwinda dhahabu ya kwanza kesho Tokyo

Mara ya mwisho kwa Kenya kushinda dhahabu ya shindano hilo ilikuwa mwaka 2015 kupitia kwa Vivian Cheruiyot.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya inapania kutwaa dhahabu ya kwanza kesho katika siku ya kwanza ya mashindano ya Roadha Duniani mjini Tokyo, Japan.

Mashindano hayo ya siku tisa yataandaliwa kati ya kesho Jumamosi na tarehe 21 mwezi huu yakiwashirikisha wanariadha zaidi ya 2000 kutoka mataifa 200.

Bingwa wa Olimpiki na mshikilizi wa rekodi ya Dunia Beatrice Chebet atawaongoza Agnes Jebet na Janeth Jepngetich kwenye fainali ya mita 10,000 kuanzia saa tisa unusu kesho alasiri.

Mara ya mwisho kwa Kenya kushinda dhahabu ya shindano hilo ilikuwa mwaka 2015 kupitia kwa Vivian Cheruiyot.

Fainali nyingine ambayo huenda iwashirikishe Wakenya ni mita 400 kwa wanariadha wanne mesto kupokezana kijiti, ikitanguliwa na mchujo.

Kenya inawakilishwa na wanariadha 58.

Share This Article