Kenya itawania kutetea taji ya wanawake ya mita 800 katika siku ya mwisho ya makala ya 20 ya mashindano ya Riadha Duniani mjini Tokyo, Japan, leo.
Bingwa mtetezi Mary Moraa atashirikiana na bingwa wa Dunia kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20 Sarah Moraa, na bingwa wa kitaifa Lillian Odira, kwenye fainali hiyo kuanzia saa saba na dakika 35 adhuhuri.
Mathew Kipchumba atakuwa Mkenya pekee kwenye fainali ya mita 5,000 kuanzia saa saba na dakika 47.
Kenya ingali ya pili kwenye msimamo wa Dunia kwa medali 10, Dhahabu 6, Fedha 2 na Shaba 2.
Marekani inaongoza kwa medali 20 (dhahabu 12, fedha 4 na shaba 4), huku Kanada ikiwa ya tatu kwa dhahabu 3 na shaba 1.