Kenya kushurutisha vipimo vya selimundu kwa watoto nchini

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya imeanzisha mikakati ya kufanya kuwa lazima vipimo vya ugonjwa wa selimundu (sickle cell) kwa watoto wote wanaozaliwa ili kupunguza visa vya maambukizi na kupata matibabu ya mapema.

Katibu wa huduma za matibabu Dkt. Ouma Oluga alisema hayo jana Jumanne katika kikao cha 80 cha Baraza la Umoja wa Mataifa (UNGA) jijini New York, Marekani, alipomwakilisha Rais William Ruto katika mkutano huo maalumu kuhusu ugonjwa wa selimundu.

Dkt. Oluga alieleza kuwa ugonjwa huo ungali donda sugu humu nchini na barani Afrika, ambapo takriban watoto 14,000 huripotiwa kuzaliwa nao nchini, huku asilimia 90 wakifariki kabla ya kutimiza miaka mitano.

Aliongeza kuwa ni kupitia kwa vipimo vya lazima kwa kina mama na watoto ambapo matibabu ya mapema yatatolewa kwa watoto wagonjwa.

Share This Article