Kenya kuandaa fainali ya CHAN,Tanzania yapewa mechi ya ufunguzi

Mechi ya ufunguzi itapigwa katika kiwara cha Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Agosti 2, wakati uchanjaa wa Mandela jijini Kampala ukiandaa mchuano wa nafasi ya tatu na nne.

Dismas Otuke
1 Min Read

Kenya imeteuliwa kuandaa fainali ya makala ya nane ya kipute cha Kombe la mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ligi za nyumbani CHAN Agosti 30 mwaka  huu katika uwanja wa kimataifa wa Kasarani.

Uamuzi huo umeafikiwa leo baada ya Shirikisho la soka Afrika kukutana na mataifa matatu yanayoandaa kipute hicjo ;Kenya,Tanzania na Uganda kati ya Agosti 2 na 30.

Mechi ya ufunguzi itapigwa katika kiwara cha Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam Agosti 2, wakati uchanjaa wa Mandela jijini Kampala, ukiandaa mchuano wa nafasi ya tatu na nne.

Aidha,uwanja wa Amaan kisiwani Zanzibar utaandaa mechi za kundi .

Timu za kundi A zitachezea Nairobi zikiwemo  Kenya, Morocco, Angola, DRC na  Zambia nazo timu za kundi B zitakita kambi  Dar es Salaam, Tanzania, zikiwa Tanzania, Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya kati.

Kundi C litakuwa Kampala likijumuisha Uganda, Niger, Guinea, Afrika kusini na  Algeria,huku kundi D likipiga kambi kisiwani  Zanzibar likiwajumuisha  Zanzibar, Senegal, Congo, Sudan na Nigeria.

Share This Article