Kenya Airways yaongeza safari za ndege kuelekea Kisumu

Tom Mathinji
1 Min Read
Shirika la Ndege la KQ laongeza safari za ndege kuelekea Kisumu mwishoni mwa wiki.

Shirika la Ndege la Kenya Airways (KQ), limeongeza  safari zake za ndege kuelekea Kisumu mwishoni mwa wiki kabla ya mazishi ya aliyekuwa Waziri Mkuu Raila Odinga siku ya Jumapili.

Kupitia ukurasa wake wa X, shirika hilo lilisema limechukua hatua hiyo, ili kuhudumia idadi kubwa ya wasafiri wanaosafiri kwenda Kisumu kwa mazishi hayo kupitia ununuzi wa tikiti nyingi.

“Tumeongeza safari zetu za ndege mwishoni mwa wiki kutokana na ongezeko la hitaji,” ilisema KQ.

KQ imesema imeongeza ndege mbili siku ya Ijumaa, moja siku ya Jumamosi, na ndege ya pili aina ya boeing 737.

Jumapili safari za ndege ya KQ654 ya saa mbili na dakika tano asubuhi na ya KQ671 ya saa moja usiku zitakuwa aina ya Boeing 737.

Vile vile safari za ndege za  KQ 654 na KQ670 za Jumatatu kutoka Kisumu zitakuwa aina ya boeing 737.

Shirika hilo la ndege limeahidi kuhakikisha abiria hawatatiziki kwenye safari zao za mwishoni mwa wiki.

Share This Article