KDF watwaa ubingwa wa mbio za kitaifa za nyika

Brilliant Jepkorir wa Magereza na Daniel Ebenyo Simiu kutoka Police waliibuka mabingwa wa mbio za kilomita 10.

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya jeshi ilitwaa ubingwa wa jumla wa makala ya mwaka huu ya mbio za kitaifa za nchi zilizoandaliwa jana katika uwanja wa michezo wa Eldoret.

KDF ilizoa alama 33 ikifuatwa na Police kwa pointi 35, wakati Magereza ikitwaa nafasi ya tatu kwa alama 53.

South Rift ilichukua nafasi ya nne kwa pointi 103, Central wakafuatia kwa alama 114.

Brilliant Jepkorir wa Magereza na Daniel Ebenyo Simiu kutoka Police waliibuka mabingwa wa mbio za kilomita 10.

Mbio hizo ambazo zilikamilisha msimu wa mbio za nyika zilishirikisha maeneo 16 yaliyo chini ya mwavuli wa chama cha Riadha Kenya.

Share This Article