Kaunti ya Mandera yapiga marufuku shughuli za chimbo

Hatua hii inafuatia kutekwa nyara kwa wachimbaji wawili wa  migodi  Jumatano katika eneo la Mandera Kusini.

Dismas Otuke
0 Min Read

Kamishna wa kaunti ya Mandera, Henry Ochako, amesitisha shughuli za chimbo katika kaunti hiyo kutokana na hatari ya kiusalama kutoka kwa kundi haramu la  wanamgambo wa Al-Shabaab.

Hatua hii inafuatia kutekwa nyara kwa wachimbaji wawili wa  migodi  Jumatano katika eneo la Mandera Kusini.

Yamkini wachimbaji migodi hao walitekwa nyara na wanamgambo wanne wa Al Shabaab, walioondoka nao kuelekea mahai kusikojulikana.

Share This Article