Kaunti tisa kuathiriwa na ukosefu wa umeme Jumatano

Tom Mathinji
2 Min Read
Baadhi ya kaunti hapa nchini kukosa nguvu za umeme.

Maeneo kadhaa hapa nchini yatakosa umeme leo Jumatano kuanzia saa mbili asubuhi, hadi saa kumi na moja jioni.

Kulingana na ilani iliyochapishwa na kampuni ya Kenya Power, ukosefu huo unatokana na shughuli za ukarabati zitakazokuwa zikitekelezwa.

Kupitia ukurasa wa X, kampuni hiyo ilitangaza kuwa kaunti zitakazoathirika na ukosefu huo wa umeme ni pamoja na Nairobi, Kakamega, Kisii, Embu, Meru, Kiambu, Kitui, Kilifi na Kwale.

Katika kaunti ya Nairobi, sehemu zitakazoathirika zinajumuisha: Barabara za Muratha, Hinga, na Gichagi, shule ya msingi ya Kangemi, ile ya upili ya Kangemi, Kangemi Bottom Line, Kangemi Shangilia, Ananda Marga Academy, Kangemi Dallas, shule ya msingi ya Kihumbuini, benki ya Kangemi Co-op Bank, na maeneo yaliyo karibu.

Maeneo mengine ni; Mtaa wa Umoja 2, Kanisa Katoliki la St. Veronicah, shule za Busara, Peter Kibukosya , Kifaru, Tumaini Primary, na maeneo yaliyo karibu.

Maeneo yatakayoathirika Magharibi mwa nchi ni pamoja na soko la Lukume, Bukhakunga, Imbiakalo, Sawasawa, Burundu, Shihome, na maeneo yaliyo karibu.

Sehemu za Kiambu zitakazokosa umeme ni,  Cytton, hospitali ya St. Peters, Gacharage, Total Gacharage, Ndenderu, Kahingo Stage, Club Decimal, Royal Brain, na maeneo yaliyo karibu.

Katika kaunti ya Kilifi, maeneo ya Mwango, Mkoroshoni, Basi, Mzongoloni, Mtondia, Tezo, Chumani, Magorani, Zowerani na Ngerenya yatakosa umeme huku maeneo ya Kwale yatakayoathiriwa yakiwa ni Vingujini, Sawasawa Beach, Msambweni Referral Hosp, Msambweni Beach House, KMTC Msambweni na maeneo yaliyokaribu.

 

Share This Article