Kassait na Kiprop waibuka kidedea mbio za Nyika za Magereza

Dismas Otuke
1 Min Read
SONY DSC

Lilian Kassait na mwanariadha aliye alikwa Festus Kiprop ndio mabingwa wa kilomita kumi wa mbio za nyika baina ya matawi ya idara ya magereza zilizoandaliwa leo katika kituo cha makurutu wa magereza mjini Ruiru.

Kassait, akiwakilisha eneo la kaskazini mashariki, alikata utepe wa kwanza katika mbio za wanawake kwa kutumia muda wa dakika 33 na sekunde 48, sekunde 5.5, mbele ya kurutu Rebecca Mwangi aliyemaliza wa pili wakati Caren Chebet wa Pwani akimaliza wa tatu kwa dakika 34 na sekunde 24.10.

Kiprop alishinda mbio za wanaume kwa muda wa 29 sekunde 47.10, akifuatwa na mwanariadha mwingine wa kualikwa Shadrack Koech aliyemaliza wa pili kwa muda wa dakika 29 sekunde 48.80 .

Simon Itot wa Bonde la Ufa akichukua nafasi tatu kwa muda wa dakika 30 na sekunde 10, naye Charles Muneria wa Kaskazini Mashariki akachukua nafasi ya nne kwa dakika 30, sekunde 15, nukta 50.

Idara ya magereza ilitumia mbio hizo kuteua kikosi chake kwa mashindano ya kitaifa ya mbio za nyika yatakayoandaliwa tarehe 25 mwezi huu katika uwanja wa michezo wa Eldoret.

Share This Article