Mechi ya Ligi Kuu Kenya ikiwa Derby Kariokoo, baina ya mahasimu wa jadi Yanga na Simba, imeratibiwa kusakatwa tarehe 15 mwezi ujao.
Usimamizi wa bodi inayoendesha Ligi Kuu ya Tanzania bara imetangaza kuwa mechi hiyo iliyoahisrishwa kutoka mwezi Machi 8 mwaka huu, baada ya Simba, kukosa kuingia uwanjani baada ya wenyeji Yanga kuwanyima fursa ya kufanya mazoezi ilivyo kidesturi kabla ya mechi kuanza.
Pambano hilo litapigwa katika uchanjaa wa Benjamin Mkappa.
Hata hivyo kungali na atiati iwapo mechi hiyo itaendelea ilivyopangwa baada ya wenyeji Yanga, kusimama tisti kuwa kamwe hawako tayari kucheza na Simba, wakiishutumu bodi na shirikisho la soka TFF kwa mapendeleo.